Every attitude, every gesture has to fight poverty and exclusion. There are many ways to act, regardless of our skills and availability. These messages, these testimonials reflect. Feel free to contribute.

Testimonies are published under the responsibility of the author. They are subject to validation: these will be published only if they comply, in form and substance the spirit of this day as defined in the International Charter for October 17.

 

Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na thamani kuliko wengine

Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na thamani kuliko wengine

Katika maandalizi ya siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini uliokithiri tulikutana na wanachama tofauti wa ATD Dunia ya Nne. Walitueleza kuhusu uwelewa wao juu ya ubaguzi, wakati walipotengwa, na namna ya kuutokomeza ubaguzi. Yafuatayoni baadhi ya maneno yao......

Mfanyakazi kutoka soko la samaki alituambia: “Ubaguzi ni hali ya kuunda matabaka. Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na thamani kuliko wengine. Wote wenye thamani, endapo wanataka kitu, wanakipata, wanaposema kitu, husikilizwa. Kwa wasiokuwa na thamani, endapo wanataka kitu, haiwezekani kukipata na wanaposema kitu, hawasikilizwi”.

Kijana kutoka Tandale alituambia “Katika nchi yetu, matajiri huwatenga watu maskini. Hufikiri watu maskini kuwa hawawezi kutoa mawazo mazuri kwasababu ya umaskini wao. Japokuwa, mawazo yao yanaweza kuisaidia jamii kuishi vizuri.”

Rafiki kutoka kundi la Tunapenda alituambia: “Watu wanao tengwa zaidi ni walemavu, hata serikali haiwajali. Jamii pia haioni kuwa ni watu wenye akili timamu na wenye kuchangia mawazo”.

Mfanyakazi kutoka soko la samaki alituambia: “Zeru zeru ni ndio watu wanaotengwa sana, japokuwa wana haki sawa ya kuishi na kupata haki zao za msingi. Ni sawa kama watu wengine. Tunatakiwa kutokomeza mawazo kuwa zeru zeru hawana thamani”.

Mama kutoka Tandale alituambia: “Hakuna elimu ambapo baadhi ya watu wana wadharau wengine. Wahajaelimika, hawajui kuwa watu wote ni binaadam na tupo sawa”.

Wafanyakazi kutoka soko la samaki alituambia: “Ni tabia ya baadhi ya watu. Baadhi ya watu matajiri hawawatengi maskini, wapo tayari kuwasaidia na kuwa marafiki zao. Lakini wapo wenye tabia mbaya huwatenga. Baadhi ya watu hujaribu kutumia nafasi zao kuwatenga wengine, na kuwatumia. Wamesahau ubinaadamu wao na wenzao pia ni binaadamu. Ni ubinafsi tu”.

Kijana mmoja kutoka Tandale alituambia: “Hakuna usawa katika familia. Ambapo mtoto wa kike anataka kuolewa, wanaume kutoka ile familia hukaa chini na kuzungumzia ndoa. Wanawake hawaruhusiwi kujiunga na mazungumzo na hukaa mbali na kikao. Ambapo chakula kinaandaliwa, kile kizuri kwanza huliwa na baba, kisha mama na watoto hufuata”.

Mama kutoka Tandale alituambia: “Wakati nilipojifungua mtoto Mwananyamala hospitali, niliulizia tangazo la mtoto wangu. Ni bure ila msaidizi wa dokta aliniambia nilipe 5,000. Sikuwa na pesa, nikaondoka. Nilirudi tena wiki moja iliyofuata, niliambia vile vile. Japokuwa, nilipokuwa pale, niliwaona baadhi ya watu wakipata matangazo bila ya kulipa. Wahudumu wa hospitali walikuwa wanawaambia watu walipe kutokana na muonekano wao”.

Mama kutoka Tandale alituambia; “Watu wengi hunitenga kwasababu ni mlemavu. Kwa mfano, naona vile namna wanavyoniangalia. Ambapo unawaomba msaada, wanakutazama chini. Huu ni ubaguzi.”

Rafiki kutoka Tunapenda alituambia: “Unatakiwa kuanza kuongeza uelewa na watoto kwanza. Hususani watu walemavu, njia moja ya kufanya hivi ni kuonyesha vipaji tulivyonavyo”.

Kijana kutoka Tandale alituambia: “Unatakiwa kuelimisha watu, kuwaonesha mfano mzuri, kama wanawake wanaweza kufanya vitu pia kama wanaume. Tunapaswa kuchangia na kubadilishana mawazo. Kipindi nilipokuwa shule, mwalimu alituweka wavulana na wasichana dawati moja, kuwachanganya wao, hii ilikuwa njia nzuri”.

Baba kutoka tandale alituambia: “Tunahitaji umoja miongoni mwa watu kwahiyo tunaweza kuifanya serikali kufanya vizuri. Kumaliza ubaguzi tunahitaji sauti kwa kila mtu”.

Translation by Hamisi Jumanne Mpana

Hamisi Jumanne Mpana